Sheria na Taratibu kwa Ujumla

MASHARTI YA MATUMIZI

Utangulizi

Tafadhali soma kwa makini Masharti haya ya matumizi (“Masharti”, “Masharti ya matumizi”) kabla ya kutumia huduma zinazotolewa katika wavuti ya Sokabet (“Huduma”)

Ili kutumia huduma hii utapaswa kukubaliana na Masharti. Masharti haya yatawahusu wale watakaotembelea wavuti hii, watumiaji na wote watakaoifikia na kuitumia huduma hii.

Kwa kuifikia na kutumia wavuti hii ya Sokabet unakubaliana kuhusika na Masharti haya. Kama hukubaliani na sehemu yoyote ya Masharti haya usitumie huduma za Sokabet. Tofauti na hapo itapelekea kufungwa kwa akaunti yako kuendana na Masharti ya wavuti ya Sokabet.

“Vigezo na Masharti” na “Sera ya Faragha” ni sehemu ya Masharti ya Matumizi na kutoztimiza, moja kwa moja itapelekea ukiukwaji wa Masharti hivyo na kinyume chake pia.

Kusitisha Huduma

Kampuni ina haki ya kusitisha mahusiano baina yake na mchezaji yeyote wakati wowote na kwa hiari ya Kampuni pekee. Kampuni pia ina haki ya kufunga au kusitisha kwa muda akaunti yako wakati wowote na kwa sababu yoyote ikiwemo ukiukwaji wa Masharti ya Matumizi.

Sheria za Utawala

Masharti haya yatasimamiwa na kufasiriwa kulingana na sheria za Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania

Ikiwa Haki ama Kigezo chochote hakitakamilishwa na Kampuni, haitahesabika kama kigezo cha haki hizo. Ikiwa Kigezo chochote na Masharti haya yatafanywa batili au yasiyo na mashiko na mahakama, vifungu vilivyobaki vya Masharti haya vitabaki kuwa na athari. Masharti haya yanaunda makubaliano yote baina yetu kuhusu Huduma zetu na kuibadilisha na kubadilisha makubaliano yoyote ya awali ambayo tulikuwa nayo na mteja kuhusu matumizi ya Huduma za Sokabet.

Mabadiliko

Tuna haki, kwa hiari yetu, kurekebisha au kubadilisha Masharti haya wakati wowote. Sababu ya kufanya Mabadiliko ya Masharti haya itaamuliwa na Kampuni

Kwa kuendelea kufikia wavuti au kutumia Huduma za Sokabet baada ya marekebisho hayo kutekelezwa, unakubali kuhusishwa na Masharti yaliyorekebishwa. Ikiwa haukubaliani na sheria mpya, tafadhali acha kutumia Huduma za Sokabet. Kukosa kufanya hivyo kunaweza kuwa na athari kama kufungwa kwa akaunti yako kulingana na Masharti ya wavuti ya Sokabet

Wasiliana Nasi.

Ikiwa una maswali kuhusiana na Masharti haya ya Matumizi, tafadhali wasiliana nasi. Taarifa za mawasiliano yetu zinapatikana katika kipengele cha “Contact” katika wavuti hii.